News Item
Image

Kuweka Ofa yako ya kuuza au kununua, chagua menu ya Soko, halafu teremka chini unapoona bei Ya Bidhaa masokoni, Ofa za Kuuza na Kununua hadi 'Weka Ofa'.

Bofya 'weka Ofa' na utapelekwa kwenye kurasa yenye fomu ya kujaza ofa yako. Hapo utakuta Jina la Fumbo lako na Simu ya Kiganjani imeshajazwa.

Chagua aina ya Ofa - Kuuza au ya Kununua.

Weka picha, kama ni ofa ya kuuza, ya bidhaa yako ili wanununuzi waweze kuiona.

Chagua bidhaa kwenye orodha ya bidhaa. kama haipo wasiliana nasi kwa fomu ya mawasiliano ili tuiongeze kwenye orodha.

Baada ya hapo weka kiasi unachotaka kuuza au kununua na vipimo vyake, mfano 100kg ni gunia la kilo mia moja na kiasi ni 200 kwa magunia 200 jumla.

Weka bei unayotaka kuuza au unayotaka kununulia.

Weka tarehe ambayo bidhaa inapatikana au inatakiwa.

Weka mahali ambapo bidhaa ipo au inatakiwa kuchukuliwa ili wahusika wa eneo waweze kujua ni wapi inatakiwa au inapatikana kuchukuliwa.

Baada ya hapo weka maelezo yoyote unayodhani yatasaidia, mfano  gredi ya bidhaa, jinsi livyohifadhiwa au kuboreshwa na kadhalika.

Kisha bofya weka ofa au kama unataka kurekebisha bofya Rekebisha ili uanze upya.

baada ya hapo unaweza kwenda kwenye menu ya Ofa Za Kuuza Na Kununa utaona ofa yako iko hewani!